GOD's Gift

GOD's Gift
My little angels

Wednesday, September 11, 2013

MAOMBI WAKATI WA UJAUZITO


(KWA WANAOAMINI KATIKA JINA LAYESU).....asieamini anakaribishwa kuonja/jaribu ujionee


MAANDIKO:ZABURI 127:3,MWANZO 1:28

VIPENGELE VYA MAOMBI

I. Damu ya Yesu(x3), Katika jina la Yesu(x3)

II. Baba wa Mbinguni,Muumba wa mbingu na nchi,ninakuabudu. Bwana,ninayakabidhi kwako 
maisha yangu na ya mtoto aliyeko tumboni mwangu ili uyatawale ,katika jina la Yesu.

III. Maendeleo yote ya mtoto huyu,ninayaacha mikononi mwako.

IV. Bwana,tupatie fedha mimi na mume wangu ili tuweze kumlea na kumtunza mtoto huyu,katika jina la Yesu.

V. Ninaagiza moto wa Roho Mtakatifu uteketeze kila mkono mbaya utakaogusa tumbo hili kwa lengo la kuharibu ujauzito huu,katika jina la Yesu.

VI. Ninalipiga upofu kila jicho lenye hila dhidi ya mtoto wanguu,katika jina la Yesu(x2)

VII. Ninabatilisha kila shmbulizi la kipepo dhidi ya mtoto wangu,katika jina la Yesu(x3)

VIII. Popote pale ambapo kuna wachawi wanaopanga kumchukua mwanangu, ninafutilia mbali jitihada zao hizo na kuamuru moto wa Roho Mtakatifu uwateketeze hadi pale watakapomwachia mwanangu,katika jina la Yesu.

IX. Ninaharibu kila hila za shetani na mwakala wake huko hospitalinni,nyumbani au popote pale,ambazo zimeandaliwa kunizuia nisijifungue salam,katika jina la Yesu (x3)

X. Ninajizamisha damuni mwa Yesu mimi na mwanangu,katika jina la Yesu.(x3)

XI. Ninatamka na kudai usalama wa maisha yangu na mwanangu aliyeko tumboni,katika jina la Yesu(x3)

XII. Ninaiffunika kwa damu ya Yesu nyumba yangu pamoja na hospitali nitakayokwenda kujifungua(itaje jina)

XIII. Ninatamka kuwa manesi na madaktari wa hospitali hii(itaje jina) watafanyika vyombo vya Mungu vitakavyonisaidia nijifungue sala,a,katika jina la Yesu.

XIV. Asante Bwana kwa kuyajibu maombi yangu,katika jina la Yesu .

Amina